Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
KOROSHO ZAIDI YA KILO MILIONI 29 ZAUZWA KUPITIA WRS MTWARA
17 Oct, 2026
KOROSHO ZAIDI YA KILO MILIONI 29 ZAUZWA KUPITIA WRS MTWARA

Jumla ya kilo 29,980,457 za korosho zimeuzwa kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala (WRS) katika minada miwili ya mwanzo tangu kuzinduliwa kwa msimu wa mauzo ya korosho 2026/27 mkoani Mtwara.

Katika Mnada wa kwanza ulifanyika Oktoba 12&13, 2026, kupitia Chama Kikuu cha Ushirika cha MAMCU, kilo 10,989,342 ziliuzwa kwa bei ya juu ya Sh 3,370 na bei ya chini ya Sh 3,110 kwa kilo.

Katika mnada wa pili uliofanyika leo, Oktoba 16, 2026, kupitia Chama Kikuu cha Ushirika cha TANECU, kilo 18,991,115 za korosho ziliuzwa kwa bei ya juu ya Sh 3,430 na bei ya chini ya Sh 3,250 kwa kilo.

Minada hiyo imeendeshwa kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, unaowezesha korosho kukusanywa, kuhifadhiwa katika ghala zilizoidhinishwa na kuuzwa kwa utaratibu rasmi wa minada. Mfumo huo unalenga kuimarisha uwazi, ushindani wa wanunuzi na kuwawezesha wakulima kunufaika na soko rasmi la mazao yao.

Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) imesisitiza umuhimu wa wakulima, waendesha ghala na wadau wengine kuzingatia viwango vya ubora wa korosho, hususan kiwango cha unyevu kisichozidi asilimia 10, pamoja na taratibu za uhifadhi na uendeshaji wa minada ili kulinda ubora wa zao hilo na kuongeza ushindani wake sokoni.

slot gacor