Leo tarehe 1 Septemba 2023 Naibu Waziri wa viwanda na biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amefunga mafunzo ya watendaji wa ghala yaliyofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro uliopo viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (katikati waliokaa) aliyekuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo ya watendaji wa ghala katika picha ya pamoja na viongozi na wahitimu. Kutoka kushoto ni mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Temeke Komredi Hamis Slim, Naibu Mrajis wa Ushirika Bw. Collins Nyakunga, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Mobhare Matinyi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw. Asangye Bangu, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw. Alex Ndikile, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Bi. Latifa M. Khamis na Katibu wa Umoja wa Waendesha ghala Bi. Doreen Njau. Waliosimama ni wawakilishi wa wahitimu wa mafunzo hayo.
Leo tarehe 28 Agosti 2023 mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba amefungua mafunzo ya watendaji wa ghala yaliyofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro uliopo viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) akiteta na wawakilishi wa Kampuni za Waendesha ghala katika maadhimisho ya siku ya ghala (Ghala Day) iliyofanyika katika viwanja vya Nanenane ,Ipuli Tabora tarehe 28 Juni 2023.
Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) akipata maelezo kuhusu utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kutoka kwa Kaimu Meneja Uratibu Huduma Bw. Erick Temu katika maadhimisho ya siku ya ghala (Ghala Day) iliyofanyika katika viwanja vya Nanenane ,Ipuli Tabora tarehe 28 Juni 2023.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt Hashil T. Abdallah (wa pili kulia) leo tarehe 24/03/2023 amezindua rasmi matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala katika zao la Iliki mkoani Morogoro. Uzinduzi huo umefanyika katika Kata ya Mhonda, Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
Elimu ya matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala umeendelea kufanyika katika Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa.
Elimu ya matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala umeendelea kufanyika katika Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa.
Elimu ya matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala umeendelea kufanyika katika Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa
Leo tarehe 19 februari 2023, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Dr. Batilda Buriani pamoja na Bw. David Mukomana, rais wa APIMONDIA Kanda ya Africa, amekutana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi ya Stakabadhi za Ghala Bw. Asangye Nicholas Bangu kwa ajili ya kutembelea Kiwanda cha kuchakata Asali kinachomilikiwa na Halmashauri ya Mji wa Sikonge Mkoani humo ikiwa ni maandalizi ya kikao maalum cha kujadili matumizi Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa kushirikiana na Soko la Bishaa Tanzania (TMX) kilichopangwa kufanyika tarehe 20 Februari 2023
Bodi ya Stakabadhi za Ghala ni taasisi iliyochini ya wizara ya viwanda na biashara. Taasisi hii ilianzishwa chini ya Warehouse Receipts Act No. 10 ya mwaka 2005 na Act No 3 ya 2015 iliyorekebishwa 2016. Kazi ya taasisi ni kusimamia na kuhamasisha matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani unaohakikisha...