KIKUNDI CHA USUME CHAJIFUNZA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA NANENANE-DODOMA
KIKUNDI CHA USUME CHAJIFUNZA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA NANENANE-DODOMA Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) imeendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali wanaotembelea banda hilo katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya John Malecela, Nzuguni mkoani Dodoma. Miongoni mwa waliopata elimu hiyo ni wanachama wa Kikundi cha Usume kinachojishughulisha na uongezaji thamani wa mazao kutoka Wilaya za Ikungi na Chamwino. Kikundi hicho kimetembelea leo Banda la WRRB, na kupata elimu ya namna Mfumo wa Stakabadhi za Ghala unavyofanya kazi, faida za kuhifadhi mazao katika maghala yaliyosajiliwa, upatikanaji wa masoko yenye ushindani, pamoja na fursa za kupata huduma za kifedha kwa kutumia mazao yaliyohifadhiwa. Akizungumza baada ya kupata elimu hiyo, Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Zena Mshana, amesema elimu waliyoipata itawasaidia kuboresha shughuli zao za uongezaji thamani wa mazao na kutumia fursa zinazotolewa kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala ili kuongeza tija na kipato.
