UKAGUZI KABLA YA MNADA WAONGEZA UAMINIFU KWA WANUNUZI NA WAKULIMA -WRRB
UKAGUZI KABLA YA MNADA WAONGEZA UAMINIFU KWA WANUNUZI NA WAKULIMA -WRRB
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Bw.Asangye Bangu amewapongeza wakulima kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa timu za ukaguzi za wilaya , ameyasema hayo wilayani Kyela Januari 05,2026 katika ziara ya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara na kueleza kuwa awali kulikuwepo na changamoto mbalimbali katika mfumo huo hususani kabla ya mazao kupelekwa kwenye minada na kugusia juu ya umuhimu wa kufanya ukaguzi wa kina wa mazao kwa kuhakikisha ubora na uwazi.
Amesema kuwa utekelezaji wa utaratibu huo umeleta matokeo chanya ambapo kwa sasa hakuna malalamiko kutoka kwa wanunuzi wala wakulima, hali inayochangia kuimarika kwa uaminifu katika mfumo na kuwa mshikamano huo ni msingi muhimu wa mafanikio na maendeleo endelevu kwenye sekta ya kilimo.
Aliongeza kuwa bodi inajitahidi kuendelea kuhakikisha wakulima wanapata huduma ambayo ni bora na kutoa wito kuwa milango ipo wazi wakati wowote na kuahidi kutoa ushirikiano lakini kuhakikisha masoko yanaongezeka zaidi.
