WADAU WA CHOROKO WAKUTANA MWANZA KUJADILI MASOKO KUPITIA STAKABADHI ZA GHALA NA MINADA YA KIDIJITALI....
WADAU WA CHOROKO WAKUTANA MWANZA KUJADILI MASOKO KUPITIA STAKABADHI ZA GHALA NA MINADA YA KIDIJITALI....
Wadau wa zao la choroko kutoka mikoa mbalimbali nchini leo Februari 04, 2026, wamekutana jijini Mwanza katika ukumbi wa mikutano wa Nyerere Gold Crest kujadili uzalishaji, uuzaji na masoko ya zao hilo kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala na Minada ya Kidijitali, huku Mwenyekiti na Mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. Said Mtanda. Mkutano huo umehudhuriwa na Wakuu wa Mikoa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mh. Martin Shigela, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mh. Anamringe Macha, ambao kwa pamoja wamesisitiza umuhimu wa kuimarisha uzalishaji na masoko ya zao la choroko kwa manufaa ya wakulima na uchumi wa taifa. Washiriki wa mkutano huo wamepatiwa taarifa fupi kuhusu hali ya uzalishaji wa zao la choroko katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Mtwara na Tabora, pamoja na mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa uuzaji wa choroko kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala na Minada ya Kidijitali kwa msimu wa kilimo wa 2024/2025. Mkutano huo pia umehudhuriwa na viongozi wa taasisi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Bw. Asangye Bangu, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Biashara Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege, Mkurugenzi wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Godfrey Malekano pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), Bi. Irene Madeje Mlola.
