NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ATEMBELEA WRRB DODOMA NA KUZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA BODI.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ATEMBELEA WRRB DODOMA NA KUZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA BODI.
Tarehe 27 januari, 2026 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Dennis Londo (Mb), ametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) zilizopo Mtaa wa Nyerere jijini Dodoma.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Londo alipokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB, Bw. Asangye Bangu, pamoja na viongozi na watendaji wa bodi hiyo, ambapo alipata fursa ya kukagua shughuli mbalimbali na kujionea mifumo ya usimamizi wa stakabadhi za ghala inayolenga kulinda maslahi ya wakulima na kuhakikisha uwazi katika biashara ya mazao.
Aidha, Mheshimiwa Londo alisisitiza umuhimu wa kuimarisha usimamizi wa mfumo wa stakabadhi za ghala ili kuongeza ufanisi wa biashara ya mazao na kuchangia maendeleo ya sekta ya kilimo na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Pamoja na hayo, Naibu Waziri alizindua rasmi Maadhimisho ya Miaka 20 ya WRRB tangu kuanzishwa kwake, na kuipongeza bodi hiyo kwa mchango wake mkubwa katika kulinda maslahi ya wakulima na kukuza biashara ya mazao nchini. Alitoa wito kwa WRRB kuendelea kuboresha mifumo yake ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya soko.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB, Bw. Asangye Bangu, alimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa ziara na uzinduzi huo, akibainisha kuwa maadhimisho hayo ni fursa ya kutathmini mafanikio na kuweka mikakati mipya ya kuimarisha Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.
