NAIBU KATIBU MKUU AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA WRRB MOROGORO
10 May, 2026
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Aristides Mbwasi amefungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Mei 8, 2026, kilichofanyika katika Ukumbi wa Edema mkoani Morogoro.
Aidha katika Kikao hicho cha Baraza pia kimejadili Bajeti ya mwaka 2026/2027 pamoja na kujadili namna bora ya kutatua kero mbalimbali za watumishi mahali pa kazi ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Bw. Mbwasi aliwasisitiza wajumbe kufanya kazi kwa utu, ushirikiano na uwajibikaji ili kuendelea kuimarisha utendaji wa taasisi pamoja na huduma zinazotolewa kwa wadau wake.
