WAKUU WA IDARA NA VITENGO WRRB WAPATIWA MAFUNZO YA UONGOZI, TATHMINI NA AKILI MNEMBA (AI)
WAKUU WA IDARA NA VITENGO WRRB WAPATIWA MAFUNZO YA UONGOZI, TATHMINI NA AKILI MNEMBA (AI)
Dar es Salaam, Februari 10, 2026
Wakuu wa Idara kutoka Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Asangye Bangu, wamehudhuria mafunzo maalum ya uongozi, tathmini na ufuatiliaji wa utendaji kazi pamoja na mafunzo ya akili mnemba (Artificial Intelligence – AI).
Mafunzo hayo yanayoendelea kufanyika kwa siku tatu, kutoka Februari 9,2026 yanatarajiwa kuhitimishwa Februari 11, 2026 jijini Dar es Salaam yamewakutanisha wakuu wa idara za Meneja Rasilimali Watu,Meneja Uratibu Huduma
Meneja Mipango na Uhamasishaji,
Mhasibu Mkuu pamoja na wakuu wa vitengo vya Ununuzi,TEHAMA,Mkaguzi Mkuu wa ndani na Sheria, yakilenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji, kuongeza ufanisi katika kusimamia majukumu yao na kuimarisha mifumo ya tathmini na ufuatiliaji wa shughuli za bodi.
Mafunzo hayo ya menejimenti ni sehemu ya mkakati wa bodi ili kuimarisha uwezo na matumizi ya teknolojia katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wadau wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala nchini.
