MHESHIMIWA HAMAD CHANDE AMEIPONGEZA WRRB, AHIMIZA UTEKELEZAJI WA KAULI MBIU YA NANE NANE 2026.
MHESHIMIWA HAMAD CHANDE AMEIPONGEZA WRRB, AHIMIZA UTEKELEZAJI WA KAULI MBIU YA NANE NANE 2026.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Hamad Chande (Mb), leo tarehe 6 Agosti,2026, ametembelea Banda la Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) katika Maonesho ya 33 ya Kimataifa ya Kilimo (Nane Nane) na kupata elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo katika kuimarisha mfumo wa stakabadhi za ghala nchini.
Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, Mh. Chande ameipongeza WRRB kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kusimamia mfumo wa stakabadhi za ghala na kuwa nyenzo muhimu ya kuwawezesha wakulima kupata masoko yenye ushindani, kuongeza thamani ya mazao yao na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa.
Aidha, ameisifu taasisi hiyo kwa juhudi zake za kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali na kubainisha kuwa hatua hiyo inasaidia kuongeza uelewa na ushiriki wa wazalishaji kwa manufaa ya maendeleo ya sekta ya kilimo.
Mhe. Chande pia ametoa wito kwa WRRB na wadau wengine kuendelea kuitekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Maonesho ya 33 ya Nane Nane isemayo, "Tambua Soko, Ongeza Tija, kutekeleza Dira 2050," kwa kuimarisha mifumo ya masoko, kuongeza tija katika uzalishaji na kuhakikisha wakulima wananufaika na fursa zilizopo katika mnyororo wa thamani wa mazao.
