Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YAFANA DODOMA
09 Mar, 2026
SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YAFANA DODOMA

Wanawake wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala leo, Machi 8, 2026, wameungana na wanawake wengine duniani kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Wilayani Kongwa, Mkoani Dodoma. 

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali, huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, na kuonesha mshikamano na ushirikiano mkubwa wa wanawake kutoka sekta tofauti katika kuimarisha umoja, usawa na haki katika jamii.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka 2026 inasema:
“Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kuelekea Dira 2050.”

Kupitia maadhimisho haya, wanawake wameendelea kuhamasishwa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi, huku wakijenga kizazi chenye misingi ya haki, usawa na fursa sawa kwa wote.