**MKUU WA MKOA WA KATAVI AZINDUA MSIMU WA MAUZO YA UFUTA NA MAZAO MENGINE KUPITIA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA 2026/2027
Leo, Mei 4, 2026, Mhe. Mwanamvua Mlindoko, Mkuu wa Mkoa wa Katavi , amezindua msimu mpya wa mauzo ya zao la ufuta na mazao mengine kupitia mfumo wa stakabadhi za ghala kwa mwaka 2026/2027.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mhe. Mlindoko amewataka wadau kuhakikisha malipo ya wakulima yanafanyika kwa wakati na kuzingatia vipimo sahihi ili kulinda maslahi yao na kuimarisha uaminifu wa mfumo.
Aidha, Bw. Asangye Bangu, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), amesema kwa kushirikiana na taasisi nyingine wataendelea kuboresha mfumo huo na kutafuta wanunuzi wengi zaidi ili kuongeza ushindani na hatimaye wakulima wapate bei nzuri.
Mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali, Pamoja na Wakuu wa Taasisi Wakiwemo Afisa Mtendaji Mkuu Soko la Bidhaa Tanzania (TMX)Bw.CPA Godfrey Malekano Pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko(COPRA) Bi.Irene Mlola ambao wamekubaliana kusimamia ipasavyo mazao yanayoingizwa kwenye mfumo, kuzuia utoroshwaji, na kuhakikisha wakulima wanalipwa kwa wakati kulingana na bei ya mnada
