Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
WIZARA, STAKABADHI ZA GHALA WAJA TANGA KUJADILI SOKO LA MWANI 
19 Sep, 2025
WIZARA, STAKABADHI ZA GHALA WAJA TANGA KUJADILI SOKO LA MWANI 

WIZARA, STAKABADHI ZA GHALA WAJA TANGA KUJADILI SOKO LA MWANI 

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala,  Bangu Asangye na  Mkurugenzi wa Ukuzaji Viumbe Maji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Dkt Nazael Madalla, kujadili maandalizi ya kuanzisha mfumo wa stakabadhi gharani kwa zao la mwani.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Septemba 17, 2025, yakilenga mfumo huo kufanya kazi katika wilaya za Pangani, Mkinga na Tanga - maeneo muhimu katika uzalishaji wa mwani na maendeleo ya uchumi wa buluu.

Mfumo wa stakabadhi ghalani unatarajiwa kuimarisha bei ya mwani, uhakika wa soko na kuondoa unyonyaji wa madalali.

Mhe Balozi Dkt Batilda, ametoa wito kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuendelea kuwajengea uwezo wavuvi wa Tanga kupitia miradi ya kiuchumi kama ufugaji wa samaki kwenye vizimba ili kuongeza kipato na kuboresha maisha yao.