**Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nzuguni B Wajifunza Kuhusu Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwenye Maonesho ya Nanenane 2026**
06 Aug, 2026
📍 Dodoma
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nzuguni B wakipata elimu kuhusu Mfumo wa Stakabadhi za Ghala (WRS) kupitia zao la kakao ambalo ni miongoni mwa mazao yanayotumia Mfumo huo katika Banda la Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Malecela, jijini Dodoma Agosti 1-8, 2026.
