Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
MAFUNZO KWA MAMENEJA DHAMANA NA WATUNZA GHALA YAFUNGULIWA RASMI MWANZA
27 Jan, 2026
MAFUNZO KWA MAMENEJA DHAMANA NA WATUNZA GHALA YAFUNGULIWA RASMI MWANZA

MAFUNZO KWA MAMENEJA DHAMANA NA WATUNZA GHALA YAFUNGULIWA RASMI MWANZA

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mhe. Arch Ng’wilabuzu Ludigija, amefungua rasmi mafunzo maalum kwa Mameneja Dhamana na Watunza Ghala leo tarehe 26 Januari 2026 katika Ukumbi wa Chuo cha Elimu ya Biashara – Kampasi ya Mwanza.

Mhe. Ludigija amesisitiza umuhimu wa mafunzo hayo katika kuimarisha weledi, uwajibikaji na uadilifu kwa wadau wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala (WRS) ili kulinda maslahi ya wakulima na kukuza uchumi wa taifa. Pia ameipongeza WRRB kwa kuendelea kutoa mafunzo yanayochangia fursa za ajira kwa vijana.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa WRRB, Bw. David Sukali, amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha wahusika wote wanazingatia sheria, taratibu na miongozo ya uendeshaji wa mfumo huo pamoja na kuboresha ubora wa mazao yanayopitia kwenye mfumo wa stakabadhi za ghala.

Mafunzo haya yanatarajiwa kufanyika kwa siku tano na yanawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo na biashara ya mazao.