Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
RAIS SAMIA AWAAPISHA WAZIRI NA NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA
19 Nov, 2025
RAIS SAMIA AWAAPISHA WAZIRI NA NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA

RAIS SAMIA AAPAISHA WAZIRI NA NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemuapisha Mheshimiwa Judith Salvio Kapinga kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara na Mheshimiwa Patrobas Paschal Katambi kuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo.

Hafla ya uapisho imefanyika Ikulu, jijini Dodoma, ikiwa imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wakiwemo Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.