Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
# SIKU YA PILI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA WRRB YAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA BIASHARA YA MAZAO NA UCHUMI WA TAIFA
18 May, 2026
# SIKU YA PILI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA WRRB YAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA BIASHARA YA MAZAO NA UCHUMI WA TAIFA

Leo Mei 18, 2026, wadau mbalimbali wamekutana katika siku ya pili ya  maadhimisho miaka 20 ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), ambapo Serikali imeeleza mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia mfumo huo katika kukuza biashara ya mazao na uchumi wa Taifa.
Mgeni Maaalum katika maadhimisho hayo alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Judith Kapinga ambaye alisema Serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya biashara, masoko ya mazao pamoja na kuongeza thamani ya mazao ya wakulima nchini.


Aidha alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi yaliyosaidia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kuendelea kuwa na mchango mkubwa katika sekta ya biashara na kilimo.
Imeelezwa kuwa tangu mwaka 2007/08 hadi Desemba 2025, zaidi ya kilogramu bilioni 5.2 za mazao 18 zenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 11.3 zimeuzwa kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, huku zaidi ya ajira 30,000 zikitokana na shughuli za mfumo huo katika mikoa 23 nchini.


Serikali pia imebainisha kuwa itaendelea kuimarisha matumizi ya TEHAMA, kuongeza uwekezaji katika maghala na kuondoa urudufu wa majukumu katika sekta za biashara ili kuongeza ufanisi na ushindani wa haki.
Wadau waliohudhuria maadhimisho hayo wameeleza kuwa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala umeendelea kuwa nyenzo muhimu ya kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara wa mazao, huku wakisisitiza ushirikiano zaidi katika kuendeleza sekta hiyo kwa manufaa ya uchumi wa Taifa.

slot gacor