SIKU YA PILI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA WRRB YAJADILI FURSA ZA BIASHARA ZA KIKANDA
18 May, 2026
Leo Siku ya ya pili ya maadhimisho ya miaka 20 ya WRRB Leo mijadala mbalimbali Inaendelea kuhusu kufungua fursa za biashara za kikanda unaendelea kufanyika huku wadau wakijadili namna ya kujiweka katika nafasi ya ushindani ndani ya masoko ya EAC, SADC na AfCFTA.
Wadau hao wameeleza kuwa ushirikiano wa kikanda unatoa nafasi kubwa kwa wafanyabiashara na taasisi kuongeza masoko ya bidhaa na huduma pamoja na kukuza uchumi wa nchi.
Aidha wamehimiza kuongeza ubora wa bidhaa na matumizi ya mifumo bora ya biashara ili kuendana na ushindani wa soko la kimataifa.
Hapo baadae Waziri wa viwanda na biashara Mhe Judith Kapinga anatarajiwa kuwa mgeni maalum katika maadhimishoo haya kwa Siku ya pili.
