Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
TANZANIA YAELEZA MANUFAA YA STAKABADHI ZA GHALA UHOLANZI
19 Nov, 2026
TANZANIA YAELEZA MANUFAA YA STAKABADHI ZA GHALA UHOLANZI

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Bw. Asangye Bangu, ameeleza manufaa ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa wakulima nchini Tanzania tangu uanzishwe kwa msaada wa Mfuko wa Pamoja wa Bidhaa (CFC).

Bw. Bangu ameeleza hayo Novemba 16, 2026, alipowasilisha uzoefu wa Tanzania katika kikao kuhusu mbinu bora za kupunguza umaskini kilichofanyika mjini The Hague, Uholanzi, kabla ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 38 wa Baraza la Uongozi la CFC.

Amesema mfumo huo unawawezesha wakulima kuhifadhi mazao yao kwa usalama, kudumisha ubora wake na kutumia stakabadhi za ghala kama dhamana ya kupata mikopo kutoka benki.

 Ameongeza kuwa mfumo huo unawasaidia kukabiliana na mabadiliko ya bei sokoni na kupata fedha za kuendesha shughuli zao za kilimo.

Mbali na Tanzania, CBI ya Uholanzi, Ubalozi wa Thailand mjini Brussels, Just Know Your Coffee Cup (JKCC) ya Uganda na One Acre Fund zimewasilisha uzoefu wao kuhusu namna ya kuwawezesha wakulima wadogo kushiriki katika minyororo ya thamani.

slot gacor