Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
WRRB YABAINISHA MKAKATI WA KUPANUA SOKO LA MCHELE
19 Nov, 2026
WRRB YABAINISHA MKAKATI WA KUPANUA SOKO LA MCHELE

Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) imeeleza mkakati wake wa kushirikiana na Shirika la Posta Tanzania kutumia mfumo wa Duka Mtandao ili kupanua fursa za masoko kwa wakulima na wafanyabiashara wa mazao mbalimbali nchini, likiwemo zao la mchele.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Mchele na wadau wa mamlaka za udhibiti kilichofanyika Novemba 18, 2026 mkoani Morogoro, Afisa Masoko wa WRRB, Milembe Dabana, amesema mfumo huo unatarajiwa kurahisisha upatikanaji wa masoko na kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara kufikia wigo mpana zaidi wa wanunuzi.

Aidha, wakulima na wafanyabiashara wameipongeza WRRB kwa mchango wake katika kuimarisha Mfumo wa Stakabadhi za Ghala unaosaidia kuboresha masoko, kuongeza kipato na fursa za ajira. Wadau hao wamesisitiza umuhimu wa kuharakisha kukamilishwa kwa mkakati wa Duka Mtandao, sambamba na kutoa elimu kuhusu matumizi yake ili kuwawezesha kunufaika na fursa za masoko ya mchele.

slot gacor