MAKAMU WA RAIS ISDORY MPANGO AMEKABIDHI ZAWADI YA MSHINDI WA PILI KWA WRRB KATIKA KUNDI LA UTENDAJI MZURI KATIKA KUTOA HUDUMA
24 Aug, 2025

Leo tarehe 23.8.2025 Mhe Dr. Phillip Is Isdori Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekabidhi zawadi ya mshindi wa pili kwa WRRB katika kundi la utendaji mzuri katika kutoa huduma. Zawad hii imetolewa jijini Arusha katika kikao kazi cha wenyeviti na wakuu wa Taasisi za Umma(CEO'S FORUM). Pichani mhe Makamu wa Rais akikabidhi zawadi kwa prof Geraldine Rasheli, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya WRRB pamoja na Bw. Asangye Bangu, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB).