ZIARA YA UWAKILISHI WA JIMBO LA MOROGORO KUSINI KATIKA BODI YA USIMAMIZI WA STAKABADHI ZA GHALA
17 Feb, 2026
Leo Tarehe 16 Februari 2026 Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Bi. Benadetha Luanda akiambatana na wakulima kutoka Jimbo Hilo wametembelea ofisi za Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi Jijini Dodoma.
Ugeni huo umefika ofisini hapo kwa lengo la kujengewa uelewa kuhusu utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala katika mauzo ya mazao mbalimbali. Wakulima wameshukuru na kupongeza namna mfumo huo unavyonufaisha wakulima na kuomba elimu zaidi iendelee kutolewa kwa wadau wengi ili kupata manufaa zaidi.
