Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
WRRB NA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI WAKUTANA KUPANUA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA KATIKA SEKTA YA MIFUGO
17 Feb, 2026
WRRB NA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI WAKUTANA KUPANUA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA KATIKA SEKTA YA MIFUGO

Bodi ya  Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Asangye Bangu imekutana na kufanya kikao cha maadhimio kuhusu kuipeleka stakabadhi za ghala upande wa biashara ya mifugo na Bw. Stephen Michael Mkurugenzi wa Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko kutoka wizara ya Mifugo na Uvuvi , leo January 17 2026, jijini  Dodoma.

Katika kikao hicho walijadili suala la ushiriki wa mfumo katika kuingiza mifugo na kujadili fursa na manufaa yatokanayo na matumizi ya mfumo huo ikiwemo kuongeza upatikanaji wa masoko yenye uhakika  kuboresha bei kwa wafugaji na  kuwezesha upatikanaji wa mikopo kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala pamoja na kupunguza changamoto za uhifadhi na ubora wa bidhaa za mifugo.

Aidha kikao hicho kiliazimia kuimarisha ushirikiano wa kitaasisi kati ya Bodi na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ikiwemo kuandaa miongozo ya utekelezaji, kufanya uhamasishaji kwa wadau wa sekta ya mifugo na kutambua mashamba yatakayikidhi viwango kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mfumo huo.

Bw Stephen Michael ameridhishwa na kazi ya awali iliyofanyika na kwa pamoja pande zote mbili wamekubaliana kulikamilisha andiko la utekelezaji ambalo pia litajumuisha wadau wote ili utekelezaji wa mfumo uwe na tija na faida kwa wadau wote.