Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
BODI YA WRRB YAFANYA KIKAO CHAKE CHA KWANZA DAR ES SALAAM
16 Feb, 2026
BODI YA WRRB YAFANYA KIKAO CHAKE CHA KWANZA DAR ES SALAAM

Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) imefanya kikao chake cha kwanza Jumamosi Februari 14, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Tanzania Investment Center (TISEZA) jijini Dar es salaam kilicho ongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo mpya Prof. Geraldine Rasheli pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw. Asangye Bangu.

Katika kikao hicho cha kwanza tangu kuzinduliwa kwake kilichojumuisha wajumbe wa kamati za bodi hiyo pamoja na Menejimenti  bodi  imepokea taarifa za kamati na kuzijadili lakini pia kutoa maelekezo kwa menejimenti ikiwa ni sehemu mojawapo ya utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo.