Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
MKURUGENZI WA WRRB ATEMBELEA KIWANDA CHA UTENGENEZAJI WA GHALA ZA KISASA
20 Nov, 2025
MKURUGENZI WA WRRB ATEMBELEA KIWANDA CHA UTENGENEZAJI WA GHALA ZA KISASA

*MKURUGENZI WA WRRB ATEMBELEA KIWANDA CHA UTENGENEZAJI WA GHALA ZA KISASA NCHINI CHINA* 

Tarehe 18/11/2025.   China.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Bw. Asangye Bangu, ameongoza ujumbe  wataalam kutoka Tanzania kutembelea kiwanda cha *Shelter Architecture Technology* kilichopo Guangdong, China. Kiwanda hicho kinajishughulisha na utengenezaji wa Ghala za kisasa zinazohamishika (Smart & Movable Warehouses).

 

Ziara hiyo imelenga kujifunza na kuangalia namna Tanzania inaweza kupata ghala za kisasa, bora na imara kwa ajili ya kuboresha Mfumo wa Stakabadhi za Ghala na kuimarisha miundombinu ya kuhifadhi mazao nchini.