WATUMISHI WA WRRB WAUNGANA NA WAFANYAKAZI WENGINE KUSHEREHEKEA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI
10 May, 2026
Leo,Mei 1,2026 watumishi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) wameungana na watumishi wengine kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani, katika maadhimisho yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Kitaifa, maadhimisho hayo yamefanyika mkoani Njombe, yakiwakutanisha watumishi kutoka sekta mbalimbali nchini kuadhimisha mchango wao katika kuleta maendeleo ya taifa
Maadhimisho hayo yamebeba Kaulimbiu isemayo “kazi zenye Staha ni Nguzo Imara Kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelesaji wa Dira ya Taifa 2050”
