BODI YA USIMAMIZI WA STAKABADHI ZA GHALA YAKUTANISHA WADAU MUHIMU KUJADILI MATUMIZI YA STAKABADHI ZA GHALA KATIKA KUIMARISHA BIASHARA YA MIFUGO
Leo, tarehe 9 Machi 2026, Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala imekutana kwa ajili ya muendelezo wa vikao vya kujadili matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala katika mauzo ya mifugo. Kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali muhimu kutoka Wizara ya mifugo na Taasisi za fedha, wakiwemo wawakilishi kutoka taasisi za kibenki, Bodi ya Nyama, TMX pamoja na Chama cha wafugaji. Lengo la kikao hicho lilikuwa kujadili na kutathmini namna mfumo wa stakabadhi za ghala unavyoweza kutumika kuboresha uwazi katika biashara ya mifugo, kuongeza thamani ya mifugo, na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wafugaji kwa kutumia mifugo yao kama dhamana. Majadiliano yaliyofanyika yameweka msingi wa kuimarisha ushirikiano kati ya wadau mbalimbali, kwa lengo la kuhakikisha mfumo huu unatumika kwa ufanisi katika kukuza biashara ya mifugo pamoja na kuinua uchumi wa wafugaji
