Afisa WRRB Aeleza Umuhimu wa Leseni kwa Waendesha Ghala
27 Mar, 2026
Afisa Leseni kutoka Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) Nasri Khea ameendelea kutoa somo la leseni kwa waendesha ghala, akieleza kwa kina umuhimu wa kuwa na leseni halali katika uendeshaji wa shughuli za ghala.
Katika mafunzo hayo amesisitiza kuwa leseni ni nyenzo muhimu inayosaidia kuhakikisha uwazi, uaminifu na ufanisi katika mfumo wa stakabadhi za ghala, huku ikiimarisha uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.
Aidha, washiriki wamehimizwa kufuata masharti yote ya leseni ili kuepuka changamoto za kisheria na kuongeza tija katika shughuli zao.
