Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
WRRB YAJIRIDHISHA NA MAANDALIZI YA UUZAJI WA MIFUGO KUPITIA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA
22 Jan, 2026
WRRB YAJIRIDHISHA NA MAANDALIZI YA UUZAJI WA MIFUGO KUPITIA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA

WRRB YAJIRIDHISHA NA MAANDALIZI YA UUZAJI WA MIFUGO KUPITIA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA

Kufuatia makubaliano ya mashirikiano kati ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) na Chama cha Wafugaji Tanzania, jana tarehe 21 Januari 2026, Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB, Bw. Asangye Bangu, alitembelea miundombinu ya mfugaji Bw. Shamba Kubwa, iliyopo Dakawa, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro.

Hatua hiyo ilikuwa na lengo la kujionea kwa karibu maandalizi yanayoendelea ya kuuza mifugo kupitia mfumo wa stakabadhi za ghala, ikiwa ni hatua muhimu katika kuboresha masoko ya mifugo na kuwawezesha wafugaji kupata thamani halisi ya mifugo yao.

Akizungumza baada ya kujionea miunro mbinu hiyo, Bw. Bangu alisema ameridhishwa na kiwango cha maandalizi kilichofikiwa hadi sasa.

“Nimeridhishwa na maandalizi hayo; kwa kweli yajayo yanafurahisha,” alisema Bw. Bangu.

Utekelezaji wa mfumo wa stakabadhi za ghala katika sekta ya mifugo unatarajiwa kuleta mageuzi chanya, ikiwemo kuongeza uwazi katika biashara, kuboresha uhakika wa masoko, na kuinua kipato cha wafugaji nchini.

Hutua hiyo ni sehemu ya juhudi za WRRB na wadau wake kuhakikisha mfumo huo unatekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa