WATUMISHI WA WRRB WAFANYA UTALII WA NDANI HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI
10 May, 2026
Leo Mei 9 2026, Bw. Asangye Bangu,Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala(WRRB) pamoja na watumishi wa Bodi hiyo wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa ajili ya kufanya utalii wa ndani na kupata muda wa kupumzika baada ya kipindi kirefu cha utekelezaji wa majukumu ya kazi. Ziara hiyo imelenga kuwajengea watumishi ari mpya ya kazi, kuimarisha ushirikiano pamoja na kuwapa fursa ya kufurahia vivutio vya utalii vilivyopo nchini. Aidha, watumishi walipata nafasi ya kujionea wanyamapori mbalimbali na mandhari ya kuvutia yaliyopo katika hifadhi hiyo.
