Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

WCF Logo
WRRB YAJIPANGA KWA MSIMU WA KOROSHO
12 Sep, 2025
WRRB YAJIPANGA KWA MSIMU WA KOROSHO

WRRB yajipanga kwa msimu wa Korosho

 Tarehe 11 Septemba 2025 Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) Asangye Bangu amefanya kikao cha ndani kwa lengo la kujipanga kuelekea msimu wa zao la Korosho, ambapo kusimamia kwa weledi na umakini kumewekwa kipaumbele.

Akiongoza kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB, Bw. Asangye Bangu, amewasisitiza watumishi kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa weledi na ubunifu mkubwa hasa usimamizi wa shughuli za ghala kwa lengo la kupata matokeo tarajiwa.

Aidha, kikao hicho kimejadili mikakati ya uboreshaji wa usimamizi wa stakabadhi za ghala, huku kikiweka msisitizo wa kuimarisha uwajibikaji na kuondoa changamoto zinazoweza kuathiri mwenendo wa msimu ujao.