Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt Hashil T. Abdallah (wa pili kulia) leo tarehe 24/03/2023 amezindua rasmi matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala katika zao la Iliki mkoani Morogoro. Uzinduzi huo umefanyika katika Kata ya Mhonda, Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
Elimu ya matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala umeendelea kufanyika katika Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa.
Elimu ya matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala umeendelea kufanyika katika Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa.
Elimu ya matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala umeendelea kufanyika katika Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa
Leo tarehe 19 februari 2023, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Dr. Batilda Buriani pamoja na Bw. David Mukomana, rais wa APIMONDIA Kanda ya Africa, amekutana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi ya Stakabadhi za Ghala Bw. Asangye Nicholas Bangu kwa ajili ya kutembelea Kiwanda cha kuchakata Asali kinachomilikiwa na Halmashauri ya Mji wa Sikonge Mkoani humo ikiwa ni maandalizi ya kikao maalum cha kujadili matumizi Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa kushirikiana na Soko la Bishaa Tanzania (TMX) kilichopangwa kufanyika tarehe 20 Februari 2023
Leo tarehe 15 Februari 2023 , Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Bw. Asangye Bangu amefanya mkutano na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo kwa lengo la kueleza majukumu ya Bodi pamoja na mipango ya utekelzaji wa mjukumu hayo.
Leo tarehe 25/01/2023, Mhe.Anthony John Mtaka - Mkuu wa Mkoa wa Njombe amekutana na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Asangye Bangu na kujadili juu ya Kuingiza mazao madogo madogo ambayo yalikuwa hayatumii Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, Mazao hayo ni Parachichi, Viazi na Mahindi.
Tarehe 24/01/2023, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Asangye Bangu amefanya ziara Mkoani Njombe kukagua miundombinu ya Ghala katika viwanda kwenye viwanda vya kuchakata zao la Chai.
Kufuatia Maelekezo ya Mhe. Hussein Mohamed Bashe (Mb) - Waziri wa Kilimo aliyotoa tarehe 18/01/2023 juu ya zao la Chai kuingizwa kwenye Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, Tarehe 24/01/2023 Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Asangye Bangu amefanya ziara Mkoani Njombe kukagua miundombinu ya Ghala katika viwanda kwenye viwanda vya kuchakata zao la Chai.
Kufuatia Maelekezo ya Mhe. Hussein Mohamed Bashe (Mb) - Waziri wa Kilimo aliyotoa tarehe 18/01/2023 juu ya zao la Chai kuingizwa kwenye Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, Tarehe 24/01/2023 Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Asangye Bangu amefanya ziara Mkoani Njombe kukagua miundombinu ya Ghala katika viwanda kwenye viwanda vya kuchakata zao la Chai.
Bodi ya Stakabadhi za Ghala ni taasisi iliyochini ya wizara ya viwanda na biashara. Taasisi hii ilianzishwa chini ya Warehouse Receipts Act No. 10 ya mwaka 2005 na Act No 3 ya 2015 iliyorekebishwa 2016. Kazi ya taasisi ni kusimamia na kuhamasisha matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani unaohakikisha...